News

Walter SIlas
Published on

Utangulizi: Historia fupi

New Life Foundation ni shirika la kikristo lenye makao yake makuu Moshi mjini, mkoani Kilimanjaro. Lilianzishwa miaka 20 iliyopita na Glorious Shoo, mchungaji wa kanisa la Assembles of God Tanzania pamoja na mke wake, Mchungaji Josephine. Watumishi hawa walianzisha shirika hili kama kuitikia wito wa mzigo wa kuwasaidia watoto maskini na yatima waliokua nao.

Safari ya New Life Foundation ilianza miaka ya tisini mwishoni wakati Askofu Glorious Shoo na mkewe, Josephine, wakiwa masomoni nchini Kenya. Waliguswa kuwasaidia watoto wanaozurura mitaani, maarufu kama “chokoraa”. Walianza kutenga sehemu ya chakula chao na kushiriki mlo wa jioni pamoja na watoto hao. Kidogo kidogo, huduma hii ilikua na baadae walianza kuwafundisha maneno la Mungu na kusali pamoja nao. Idadi ya watoto iliongezeka siku baada ya siku na baadae, watu waliguswa na huduma yao na kuanza kutoa msaada wa chakula, nguo, na mahitaji madogo madogo. 

151146118 10159500339396522 5524307128170205801 n-369-963

Baada kuhitimu, walirudi Tanzania na kuendelea na majukumu yao ya uchungaji. Hata hivyo, kutokana na mzigo walionao, walianzisha tena huduma kwa watoto, wakijikita zaidi kusaidia watoto yatima na wanatoka kwenye hali duni. Walianza kuchukua watoto wasio na wazazi/ walezi wala makazi na kuishi nao kwenye nyumba waliokua wamepanga maeneo ya Maili-sita, Moshi. Baada ya miezi kadhaa idadi ya watoto waliongezeka na walianza kuwafundisha masomo ya chekechea wakiwa hapo. Hatimae mwaka 2001, New Life Foundation ilisajiliwa rasmi kama shirika la kikristo linalotoa huduma za jamii hususani kwa watoto yatima na wale wanaotoka kwa familia duni. Hata hivyo, shirika la New Life Foundation limegusa makundi mengine katika jamii yanayohitaji msaada.

New Life Foundation ina idara kuu nne:

 

Fountain of Love:

Kituo kinachotoa huduma ya elimu na mafunzo yanayolenga malezi kwa watoto na utumishi wa kazi za kijamii. Kituo hiki pia kinajihusisha na huduma mbali mbali za kikristo, ikiwemo kufanya na kuratibu mikutano ya injili na kutoa mafundisho ya kiroho.

Fountain of Love

Fountain of Zoe:

Kituo cha kulelea watoto yatima na wale waliotelekezwa na wazazi wao katika umri mdogo.

Fountain of Zoe

Fountain of Joy:

Shule ya ufundi na stadi za kazi inayowalenga mabinti wanaotoka katika mazingira hatarishi. Mfano unyanyasaji wa kijinsia, umaskini wa kupindukia, ndoa za utotoni, ukahaba, madawa ya kulevya nk.

Fountain of Joy-332

Fountain of Hope:

Shule ya kikristo inayootoa elimu bora kwa lugha ya kiingereza kuanzia ngazi ya awali (nursery) mpaka sekondari (kidato cha nne). Zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi wanaosoma Fountain of Hope ni yatima au wanaotoka kwenye mazingira magumu.

 

Fountain of Hope

Tokea kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, New Life Foundation imegusa maisha ya watoto yatima na masikini zaidi ya elfu moja, na kusaidia mabinti Zaidi ya 100 waliotoka kwenye maisha hatarishi. Kituo cha kulelea watoto yatima cha Fountain of Zoe, kimekuza zaidi ya wachanga 50 waliotelekezwa au kufiwa na wazazi katika umri mdogo sana. Kituo cha mafunzo cha Fountain of Love kimefanya semina za mafundisho zaidi ya elfu moja nchi nzima. Watumishi wa mashirika mbali mbali kama Compassion International, World Vision, na makanisa wamenifaika kwa kiasi kikubwa na programu za Fountain of Love.

 

Shule ya Fountain of Hope Christian Primary

Shule ya awali ya Fountain of Hope ilianza kupokea watoto wa chekechea mnamo mwaka 2001 na kufanikiwa kuhitimisha kwa mara ya kwanza darasa la saba mwaka 2007. Tokea 2007, shule ya Fountain of Hope imekua ikihitimisha wanafunzi kila mwaka na mwaka huu, tutafanya mahafali yetu ya kwanza mnamo tarehe 25 mwezi Septemba.

 

Wahitimu wetu wa darasa la saba wamekua na ufaulu mzuri na dhabiti kwa miaka yote 15 tuliyotoa wahitimu. Shule ya Fountain of Hope Primary School imekua na ufaulu wa kipekee kwenye somo la hisabati na kiingereza katika mkoa wa Kilimanjaro, licha ya mkoa kuwa kati ya mikoa yenye ufaulu mzuri nchini. Wanafunzi wetu wamekua wakionesha ustadi mkubwa wa kujiamini na kujielezea kwa lugha ya kiingereza hata kuwashangaza wazazi kipindi cha likizo.

 

Shule ya sekondari ya Fountain of Hope

Shule ya Fountain of Hope Sekondari ilianza rasmi mwaka 2008 ikiwa na wanafunzi 40 wa kidato cha kwanza. Shule imeendelea kupokea wanafunzi wa sekondari kila mwaka baada ya hapo na mwaka huu tunatarajia kufanya mahafali ya tisa ya kidato cha nne mnamo tarehe 25 Septemba. Wanafunzi wetu wa kidato cha nne wamekua wakionesha ufaulu wa kipekee wakishika nafasi za kumi bora katika mkoa wa Kilimanjaro kwa miaka yote tisa mfululizo. Wanafunzi wetu wamekua na ufaulu wa kipekee katika masomo ya hisabati, sayansi na kiingereza. Mwanafunzi wetu alishika namba moja kitaifa katika somo la hisabati na kupewa cheti cha pongezi kutoka Chama Cha Hisabati Tanzania. Mnamo mwaka 2018, mwalimu wa hesabati kutoka shule ya sekondari ya Fountain of Hope alipewa cheti cha pongezi kutoka Chama Cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) kutokana na ufaulu wa juu wa wananafunzi katika somo la hisabati. Wanafunzi wa New Life Foundation waliibuka kidedea kwenye shindano la kimataifa la "Young Scientist" lilihusisha shule zaidi ya elfu mbili.

Wanafunzi wa Fountain of Hope wakiwa na tuzo Young Scientist

 

Wanafunzi wanaohitimu New Life Foundation wamekuwa mfano wa kuigwa popote waendapo katika bidii, ustadi wa kazi, na uchaji wa Mungu. Wahiitimu wa Fountain of Hope wamepokea ufadhili (scholarships) kadha wa kadha wa kusomea fani mbali mbali nje na ndani ya nchi katika Nyanja za uhandisi, biashara, teknolojia, na udaktari. Hata sasa baadhi ya wahitimu wetu wapo katika vikubwa nchini za Marekani, Urusi, India, na Uchina wakijiendeleza kimasomo.

Paul on his graduation-228

Maono ya New Life Foundation juu ya watoto

Maono ya New Life Foundation ni kukuza kizazi cha watu wataokuja kuleta mabadiliko katika miaka ijayo. Kutokana na maono haya, New Life Foundation imedhamiria kutoa maarifa yaliyojikita katika neno la Mungu (Biblia) ili kufanikisha azma ya sehemu ambapo waleta mabadiliko wanabadilishwa.

 

Tunaamini kwamba badiliko la kweli linatokea moyoni kwa mtu, na hii huja kwa kusikia neno la Mungu. Ndio maana tunafundisha watoto wetu, kusikiliza sauti ya Mungu na kutii neno lake tangu wakiwa wadogo” – Rev. Glorious Shoo, Rais na mmoja wa waanzilishi wa Shirika la New Life Foundation.

Fountain of Hope 3 44-min-953

Waalimu, walezi, na watumishi wote wa New Life Foundation ni wakristo waliookoka na kujazwa Roho Mtakatifu. Angalau mara mbili kila mwaka shirika hufanya mafundisho na semina kwa wafanyakazi wote yanayolenga namna ya kulea na kuishi na watoto.

 

Tunaamini kwamba ili mtu aweze kumbadilisha mwingine, lazima na yeye awe amebadilishwa kwanza. Ndio maana tunakua makini sana kwenye wafanyakazi tunaowachukua na mafundisho tunayowafundisha” – Rev. Glorious Shoo, Rais na mmoja wa waanzilishi wa Shirika la New Life Foundation.

Fomu za kujiunga kidato cha kwanza

 

Kipaombele cha shirika ni kusaidia yatima na watoto wanaotoka katika mazingira hatarishi, hata hivyo, takribani asilimia 30 ya wanafunzi wetu ni watoto wanaotoka kwenye familia zinazojiweza na hulipa ada kamili. Fedha hizi, pamoja na ufadhili tunaopata zinasaidia kuendesha shughuli kadhaa za shirika na kilipa wafanyakazi wake. Kama ilivyo utaratibu wa shule nyingi za binafsi, huwa tunatangaza nafasi za masomo kwa muhula mpya, na kufanya usaili wa watahiniwa.


Hivyo basi, tunayofuraha kutangaza kwamba fomu za kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka 2022, zitaanza kutolewa rasmi tarehe 23 Novemba 2021.
 

  1. Kwa mkoa wa Dar Es Salaam, fomu zinapatikana Gazeti la Jibu La Maisha, TAG Makao makuu.
  2. Mkoa wa Arusha, fomu zitapatikana Maranatha Christian Center, Mianzini
  3. Mkoa wa Kilimanjaro, Fomu zitapatikana shuleni Maili-sita na kanisa la TAG KICC Moshi

Fomu zitapatikana kwa gharama ya shilingi elfu kumi na tano tu (15,000 Tshs).

Usaili utafanyika katika tarehe zifuatazo,

  1. Mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 23 Octoba 2021
  2. Mkoa wa Kilimanjaro, tarehe 30 Octoba 2021

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo 0769 590 511 au 0678 715 009. Au tembelea tovuti yetu www.newlifetz.com